Sheikh Jalala amesisitiza kuwa Taq'wa ni msingi wa maisha ya Muumini, hasa katika nyakati tukufu kama za Eid al-Adh'ha. Aliwahimiza Waumini kuendeleza Taq'wa ili kuepuka maovu na kuishi kwa uadilifu, haki, na nidhamu ya Kiislamu.

7 Juni 2025 - 14:25

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo tarehe 6 Juni 2025 – Katika Khutba ya Swala ya Eid al-Adh'ha iliyoswaliwa katika Masjid Ghadir, Kigogo Post, Dar es Salaam, Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'asharia Tanzania (T.I.C Taifa), alisisitiza umuhimu wa Taq'wa (kumcha Mwenyezi Mungu) katika maisha ya kila siku.

Maulana Sheikh Hemedi Jalala Ahimiza Taq'wa Katika Khutba ya Swala ya Eid al-Adh'ha + Picha

Akiwasilisha Khutba yake yenye maudhui hii: “Umuhimu wa Taq'wa Katika Masiku Haya,” Sheikh Jalala alieleza kuwa khofu ya Mwenyezi Mungu (SWT) humfanya Muumini kuwa mwenye kukinai hata kwa kidogo anachokipata, na kwamba kukosekana kwa hali hiyo hupelekea watu kujihusisha na ufisadi na uharibifu.

Amesisitiza kuwa Taq'wa ni msingi wa maisha ya Muumini, hasa katika nyakati tukufu kama za Eid al-Adh'ha. Aliwahimiza Waumini kuendeleza Taq'wa ili kuepuka maovu na kuishi kwa uadilifu, haki, na nidhamu ya Kiislamu.

Eid al-Adh'ha, ikiwa miongoni mwa sikukuu muhimu zaidi kwa Waislamu duniani, huadhimisha utiifu wa Nabii Ibrahim (AS) kwa Mwenyezi Mungu. Hapa Tanzania, ni siku ya mapumziko ya kitaifa ambapo waumini hushiriki katika ibada, dua, na utoaji wa sadaka.

Maulana Sheikh Hemedi Jalala Ahimiza Taq'wa Katika Khutba ya Swala ya Eid al-Adh'ha + Picha

Eid Mubarak kwa Waislamu wote

Your Comment

You are replying to: .
captcha